Sengerema FM

Wanafunzi wachapwa viboko 75 kwa tuhuma za kufanya mapenzi shuleni

25 March 2024, 6:52 pm

Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wakizungumza na wanafunzi wanao daiwa kuchapwa viboko 75 na walimu wao kwa tuhuma za kufanya mapenzi shuleni.Picha na Emmanuel Twimanye.

Kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu mwilini pamoja na vifo ni matukio mbalimbali yaliyotendwa na yanayoendelea kutendwa dhidi ya wanafunzi huku sababu kubwa ikihusisha adhabu ya viboko jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, utolewaji wa adhabu hizo haufuati taratibu, kanuni pamoja na miongozo husika iliyowekwa

Na:Emmanuel Twimanye

Wanafunzi 12 katika shule ya  Sekondari Ipandikilo  Iliyopo Kata ya Ngoma B  Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza   wamedaiwa   kuchapwa viboko 75 na baadhi ya walimu wa shule hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi shuleni.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wanafunzi wakiwa  katika kituo cha afya  Ngoma B  wamesema kuwa baada ya kutuhumiwa kujihusiha na mapenzi , walimu walianza kuwachapa viboko kwa zamu na kupelekea  kupata maumivu makali   sehemu mbalimbali za miili yao .

Sauti ya baadhi ya Wanafunzi waliopigwa na walimu wao shuleni

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaodaiwa  kuchapwa viboko  wamesikitishwa na  tukio hilo na kuiomba serikali kuwaondoa shuleni hapo  walimu  walio tekeleza kitendo hicho.

Sauti ya Wazazi wa watoto wanao daiwa kupigwa na walimu wao

Mkuu wa shule ya sekondari Ipandikilo  Mwl, John Paul amekiri kutokea kwa tukio hilo  na kwamba wameshirikiana na afisa mtendaji wa kata hiyo kuwapeleka kwenye kituo cha afya wanafunzi hao kwa ajili ya kupatiwa matibabu wakati  taratibu nyingine zikiendelea.     

Sauti ya Mkuu wa shule ya sekondari Ipandikilo  Mwl, John Paul

Mganga mfawidhi wa  Kituo cha afya Ngoma B  Abtwalib Nkwaje  amethibitisha kuwapokea  wanafunzi  katika kituo hicho cha afya huku wakiwa na michubuko sehemu mbalimbali za milii yao. 

Sauti ya Mganga mfawidhi wa  Kituo cha afya Ngoma B  Abtwalib Nkwaje

Afisa mtendaji wa kata ya Ngoma B    Emily John  amekiri   Ofisi yake kupokea   malalamiko kuto0ka kwa wazazi wakiwa na watoto wao  wakilalamikia kupewa adhabu zilizokithiri na kuchukua hatua za kumwita mkuu wa shule hiyo  ili kutoa maelezo juu ya  tukio hilo.

Sauti ya Afisa mtendaji wa kata ya Ngoma B    Emily John

Diwani wa kata ya Ngoma B   Mh,Donald Masindi  amesema kuwa kitendo hicho hakiwezi kuvumiliwa na kushauri walimu wanaodaiwa kufanya kitendo hicho kuchuliwa hatua za kinidamu.

Sauti ya Diwani wa kata ya Ngoma B   Mh,Donald Masindi

Kufuatia tukio hilo  Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema Jackson Mazinzi  na katibu wa Jumuiya hiyo Jamal  Athuman  wamewatembelea wanafunzi katika kituo hicho cha afya na kuagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mkuu wa shule hiyo ili kukomesha vitendo hivyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM (W) Sengerema Jackson Mazinzi  na katibu wa Jumuiya hiyo Jamal  Athuman

Kwa mjibu wa kanuni ya The Education (Corporal Punishment) Regulation G.N.294 ya mwaka 2002 inatoa mwongozo ni wakati gani adhabu ya viboko inatakiwa kutolewa na kwa kiwango gani na kanuni ya 3 (1) inasema adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhabu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule heshima pia Kanuni ndogo ya (2) inasema adhabu ya viboko itolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko 4 kwa tukio lolote.