Sengerema FM

Marufu pikipiki za Samia kuendeshea bodaboda

19 April 2024, 11:37 am

Katibu wa Umoja wa wanawake (UWT ) chama cha mapinduzi (CC)Wilayani Sengerema  Rosemary Mwakisalu akitoa onyo hilo.Picha na Emmanuel Twimanye

Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Sengerema kimegawa pikipiki kwa viongozi wake wa kata na matawi ili kuwarahisishia kazi zao za kichama.

Na:Emmanuel Twimanye

Viongozi  wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza  waliopatiwa pikipiki na chama hicho  wamepigwa marufuku kuzitumia pikipiki hizo kufanya Bodaboda.

Agizo hilo limetolewa na katibu wa Umoja wa wanawake (UWT ) Wilayani Sengerema  Rosemary Mwakisalu wakati akitoa salamu za Jumuiya ya umoja huo  katika mafunzo ya usalama barabarani  kwa viongozi wa chama hicho waliopatiwa  pikipiki na chama cha mapinduzi.

Amesema kuwa Pikipiki hizo zimetolewa na mweneyekiti wa chama cha mapinduzi   (CCM)  Taifa  Mh, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi kwa  viongozi wa chama hicho hususani makatibu na si vinginevyo.

Sauti ya katibu wa Umoja wa wanawake (UWT ) Wilayani Sengerema  Rosemary Mwakisalu

Mkurugenzi wa Chuo cha Udereva Muungano Sengerema Donald Ngadaya amesema kuwa viongozi hao waliopewa pikipiki walikuwa hawana uelewa kuhusiana na masuala ya sheria na alama za  barabarani   ambapo tayari wamewafundisha  na kuelewa huku akitarajiwa watakuwa maderreva bora

Sauti ya mkurugenzi wa Chuo cha Udereva Muungano Sengerema Donald Ngadaya

Naye Mkuu wa usalama barabarani Wilayani Sengerema Hamis Wembo amewataka madereva hao kwenda kuwa mabalozi  kwa   kuzingatia sheria za usalama barabarani  kutokana na mafunzo waliyoyapata.

Sauti ya mkuu wa usalama barabarani Wilayani Sengerema Hamis Wembo

Nao baadhi ya viongozi waliopata fursa ya mafunzo hayo wameahidi kutokwenda kuzitumia pikipiki hizo kwa shughuli za bodaboda huku wakiahidi kwenda kuzingatia mafunzo hayo ili kuepuka ajali za barabarani.

Sauti ya Baadhi ya viongozi wa chama waliopewa mafunzo ya usalama barabarani

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM)  Taifa Mh,Dkt Samia Suluhu Hassan alitoa pikipiki kwa viongozi wa chama cha mapinduzi Hususani makatibu ili kurahisisha utendaji kazi wa shughuli za cha hicho.