Sengerema FM
Sengerema FM
29 July 2026, 8:14 pm

Kufuatia uwepo wa matukio ya uvunjifu wa amani katika jamii wananchi wametakiwa kushirikiana na jeshi la polisi katika wilaya ya Sengerema.
Na,Elisha Magege
Wananchi wametakiwa kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za uharifu na waharifu ili kuinua shughuli za maendeleo katika jamii.
Akizungumza na wananchi kata ya Buzilasoga mratibu wa polisi Jamii wilaya ya Sengerema ASP. Valentine Filimon Sarakikya, wakati wa zoezi la kufanya usafi katika kituo cha afya Kanyerere amesema ili wananchi wapate maendeleo wanahitaji utulivu na amani, hivyo ni vyema jamii kuwafichua waharifu na kutoa taarifa za uharifu mapema.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Buzilasoga Bi.Edina Bandihai Amelipongeza jeshi la polisi kwa kufika na kutoa elimu ya ulinzi shirikishi, huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamelishukuru jeshi la polisi wilaya ya Sengerema kwa kufika na kujumuika nao katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira.
Jeshi la Polisi wilaya ya Sengerema linaendelea na falsafa yake ya kuwaweka pomoja, polisi na jamii katika mashirikiano ya kuleta maendeleo.
