Sengerema FM

OCD awataka waendesha bajaj kuwa waadilifu na wazalendo

8 September 2026, 11:37 am

Mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Sengerema, SSP. Kurwa Misogalya akizungumza.Picha na Elisha Magege

Jeshi la polisi wilayani Sengerema limezungumza na vijana wanaojishughulisha na usafirishaji wa abilia hasa bajaji na kuwakumbusha kuwa wazalendo kwa nchi yao.

Na,Elisha Magege

Vijana wilayani Sengerema wametakiwa kuwa waadilifu na nidhamu kwa jamii inayowazunguka.

Wito huo umetolewa na mkuu wa jeshi la polisi Sengerema, SSP. Kurwa Misogalya wakati akizungumza na vijana wanao jishughulisha  na udereva bajaji,ambapo nakusema kuwa kijana wa kitanzania unatakiwa kuwa mzalendo na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo yako.

Sauti ya mkuu wa jeshi la polisi Sengerema, SSP. Kurwa Misogalya

Kwa upande wake Mkuu wa operation trafic na msaidizi wa mkuu wa usalama barabarani Sengerema Inspt. Norshid Rashid amewataka vijana wanao jishugulisha  na udereva wa kubeba abilia kuwa na nidhamu na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Sauti ya Mkuu wa operation trafic na msaidizi wa mkuu wa usalama barabarani Sengerema Inspt. Norshid Rashid

Naye mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Sengerema ASP Shabani Mbwana amewataka waendesha bajaji kuunda umoja wenye nguvu utakao wasaidia kujikwamua kimaisha.

Sauti ya mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Sengerema ASP Shabani Mbwana

Nao baadhi ya madereva bajaji wamelishukuru jeshi la polisi kwa kuwapa elimu ya uzalendo na kuzingatia sheria za usalama wawapo kazini.

Sauti za baadhi ya waendesha Bajaj wilayani Sengerema