Sengerema FM

Sengerema yapanda miti elfu 20 kumbukizi ya kuzaliwa SSH

27 January 2024, 6:48 pm

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga na viongozi wa halmashauri hiyo katika zoezi la upandaji miti kama kumbukumbu ya kuzaliwa rais Dr.Samia 2024. Picha na Elisha Magege

Tarehe 27 ya Mwezi Januari kila mwaka tangu 1960 ni kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hasani, ambapo kwa mwaka huu 2024 anatimiza umri wa miaka 64

Na; Elisha Magege

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga amewaongoza viongozi na wananchi wilayani hapo kupanda miti kama kumbukizi ya  siku ya kuzaliwa kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suruhu Hasan.

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga akipata maelekezo ya miti ili kuipanda kama kumbukizi ya kuzaliwa rais dr Samia kutoka kwa Meneja Tfs Sengerema. Picha na Elisha Magege

Akizungumza Wakati wa Zoezi hilo Mh. Senyi amesema Viongozi wa wilaya kwa kushirikiana na wakala wa misitu nchini TFS wamepanda jumla ya miti elf.20 ambapo ni miti elf 10 kwa kila Halmashauri huku lengo likiwa ni alama ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais Samia mwaka huu wa 2024.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga

Kwa upande wake Meneja wa Tfs Sengerema Bwn. James Aloise Amewataka wananchi kuendelea kutumia fursa ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini kwa kupanda miti ili kutunza mazingira na kwa manufaa yao ya badae.

Sauti ya Meneja wa Tfs Sengerema Bwn. James Aloise

Wakiwa katika kituo cha Afya Kanyerere Mganga mkuu wa Halmashauri ya Sengerema Dr. Fredrick J.Mgalula amewashukuru viongozi wa Wilaya kwa kupanda miti kwenye maeneo ya Hospitali na vituo vya Afya.

Sauti ya Mganga mkuu wa Halmashauri ya Sengerema Dr. Fredrick J.Mgalula