Sengerema FM

37 wakutwa na kipindupindu Sengerema

1 February 2024, 3:12 pm

Mkuu wa wilaya ya Sengerema akizungumza na wananchi kuchukua tahadhali ya kipindupindu mjini Sengerema. Picha Makitaba

Licha ya Serikali kutoa vifaa tiba na kinga vyenye thamani zaidi ya Sh milioni 7 kwenye mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu pamoja na dawa za kutibu maji kwa kuua wadudu wenye vimelea vya ugonjwa huo bado changamoto inazidi kuwa kubwa hasa maeneo ya kandokando ya ziwa victoria.

Na:Emmanuel Twimanye

Zaidi ya watu 37 wameripotiwa kuugua ugonjwa wa Kipindupindu Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza .

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Nganga January 31 2024 ambapo amesema kuwa watu hao waliougua  ugonjwa  huo wamelazwa  katika Kituo cha afya Katunguru ,Kituo cha Ngomamtimba na Hospitali teule ya wilaya ya Sengerema  kwa ajili ya kupatiwa matibabu .

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga akitoa takwimu za wagonjwa wa kipindupindu wilayani Sengerema

Kufuatia uwepo wa ugonjwa huo Wilayani humo Mkuu wa wilaya amewatahadharisha wananachi kuacha kusalimia kwa kushikana mikono pamoja na kuendelea kufanya usafi  wa mazingira katika maeneo yao ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga akitoa tahadhali kwa wananchi

Nao baadhi ya wananchi wilayani humo wameahidi kuchuakua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Wananchi wakizungumzia tahadhali ya kipindupindu