Sengerema FM
Sengerema FM
23 May 2026, 7:52 pm

Kutokana na kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya wananchi juu ya huduma za afya kutokizi vigezo,watumishi wa zahanati ya Busulwagili Wilayani Sengerema wamepongezwa kwa huduma bora kwa wananchi.
Na, Emmanuel Twimanye
Watumishi wa Zahanati ya Busulwangili kata ya Tabaruka Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wamepongezwa kwa kutoa huduma bora ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kuzuia vifo vya akinamama wajawazito na watoto.
Akizungumza katika ziara ya kukagua hali ya utoaji wa huduma kwa wananchi katika zahanati hiyo, Diwani wa kata ya Tabaruka Sospeter Busumabu amewapongeza watumishi wa zahanati hiyo kwa kuwahudumia wananchi vizuri.
Awali akitoa taarifa ya utoaji huduma, mganga mfawidhi wa zahanati ya Busulwangili Onesmo Patrick amesema kuwa zahanati hiyo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya Mama, Baba na mtoto.
Naye muuguzi mkuu wa zahanati hiyo Cafren Shilatu amesema kuwa wamefanikiwa kuzuia vifo vya akinamama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua kutokana na ufuatiliaji pamoja na kutoa elimu kwa akinamama na wenza wao juu ya umhimu wa kuhudhuria kliniki.
Kwa upande wao Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Tabaruka Revocatus Kaswahili pamoja na Katibu wa chama hicho wa kata hiyo Lucas Seleman wameungana na diwani kuwapongeza watumishi wa zahanati hiuo kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Baadhi ya Akinamama wajawazito na wenza wao wamefurahishwa na huduma kutoka kwa watumishi wa zahanati hiyo na kuwaomba kuendelea na moyo huo wa kuwajali na kuwahudumia kwa wakati.