Sengerema FM

Azua taharuki akidhaniwa kuwa mchawi kanisani

30 October 2023, 9:10 pm

Mwanamke anayedhaniwa kuwa mchawi akiwa kanisani .Picha na Emmanuel Twimanye

Matukio ya watu kudhaniwa kuwa wachawi yamezidi kushika kasi wilayani Sengerema ambapo mwanzoni mwa mwaka huu 2023 wanawake wanne waliodhaniwa kuwa ni wachawi walikamatwa eneo la Mwabaruhi mjini Sengerema.

Na:Emmanuel Twimanye.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida , Mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30,  anayesadikiwa kuwa ni  mchawi   amekwama ndani ya kanisa la Ebezeza Wilayani Sengerema wakati akidaiwa kujaribu kufanya jaribio la kishirikina.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamesikitishwa na tukio hilo na kusema kuwa awali  alifika mbwa kanisani hapo  na kumfukuza na  kwamba  wakati ibaada inaelekea  mwishoni ghafla mwanamke  huyo alitua  kanisani akiwa na chungu ,konono na vitu vinavyosadikiwa  kuwa ni dawa kwenye mkoba wake  kisha kuanza kumshambulia mchungaji.

Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wameshangazwa na tukio hilo na kuishauri jamii kuachana na vitendo vya Imani za kishirikina kwa kuwa vinarudisha nyuma maendeleo.

Mchungaji wa Kanisa la  Ebeneza  Ashery  Olongai  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na  kuiomba jamii  kuachana na masuala ya Imani za kishirikina na kumrudia mwenyezi Mungu.

Hata hivyo mwanamke  huyo hajafahamika ni mkazi wa wapi ambapo hadi sasa amezuiliwa katika kanisa hilo kwa ajili ya hatua zaidi.

Taarifa ya Emmanuel Twimanye ikifafanua zaidi