Sengerema FM

Wazazi walalamikiwa kushindwa kulipa Ada za watoto wao

30 October 2023, 9:02 pm

Mgeni Rasimi Bwn.Issa Shedaha kwenye mahafari ya kidato cha nne shule ya Sekondari Ntunduru Sengerema. Picha na Joyce Rollingstone.

Shule ya Sekondari Ntunduru imekuwa ikifanya vizuri tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004, ambapo kwa mwaka huu 2023 jumla ya wahitimu 70 wanatarajia kufanya mtihani wa kidato cha nne wakiwa wasichana 37 na wavulana 33.

Na:Joyce Rollingstone.

Shule ya sekondari ntunduru iliyopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo wazazi kushindwa kuwalipia ada wanafunzi kwa wakati, haliambayo inapelekea wanafunzi kusoma kwa hofu.


Hayo yamesemwa na mkuu wa shule ya sekondari ntunduru Mwl,Tibalugaziha M. Tibendelana wakato akisoma risala ya shule kwa mgeni rasmi katika mahafari ya kumi na saba ya shule hiyo tangu kuanzishwa mwaka 2004,nakusema kuwa licha ya kuwa na changamoto hizo wanafunzi wamekuwa wakifanya vizuri katika mitihani yao nakuifanya shule hiyo kuwa vizuri kitaluma.


Naye mkurugenzi wa shure hiyo bwan Madaha Richard Ntunduru Mchele amewapongeza wazazi kwa kuwaleta watoto wao katika shule ya ntunduru ili kuwaandalia msingi imara wa kielimu huku akiwapongeza wahitimu hao ,kwakuwa na nidhamu nzuri inayowafanya kuwa na matokeo mazuri katika mitihani yao.

Taarifa ya Joyce Rollingstone inafafanua zaidi