Sengerema FM

Taka zarundikwa kwenye makazi ya watu mjini Sengerema

30 January 2024, 2:13 pm

Baadhi ya wakazi wakiwa kwenye eneo la makazi yao linalodaiwa kumwangwa taka na wafanya usafi wa mji wa Sengerema. Picha na Emmanuel Twimanye

Mji wa Sengerema kwa mda mrefu umekuwa ukionekana kuwa na mrundikano wa uchafu kwenye vizimba vilivyopo mjini ambapo Halmashauri imekuwa ikitumia vibarua kuzizoa na baadhi yao wamekuwa wakitoa kwenye vizimba na kwenda kuzimwaga kwenye makazi ya watu.

Na:Emmanuel Twimanye

Wakazi wa eneo la Bujora  Mtaa wa Misheni Kata ya Misheni wameilalamikia Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza  kwa kumwaga taka karibu na makazi yao  hali inayohatarisha usalama wa afya zao  hususani katika kipindi hiki cha mlipuko wa  ugonjwa wa Kipindupindu.

Wametoa malalamiko hayo wakati wakizungumza na Radio Sengerema katika eneo hilo na kusema kuwa wanashangazwa na kitendo cha serikali inayohamasisha wananchi kujikinga na kipindupindu ili hali yenyewe ndiyo chanzo cha kuchafua mazingira kwa kumwaga taka karibu na makazi yao.

Sauti za Wananchi wakilalamikia kurundikwa kwa uchafu kwenye makazi yao

Baadhi ya watoto wameeleza kuwa uwepo wa taka hizo zimesababisha athari kwao ikiwa ni pamoja na kuugua tumbo na kukatwa na chupa pindi wanapopita katika eneo hilo.

Sauti za baadhi ya Watoto wa eneo hilo wanaopata changamoto ya uchafu

Balozi wa eneo hilo  Samwel Lubinza Fimbo  amekiri kumwaga taka hizo karibu na makazi ya watu na kwamba licha ya kumtaarifu mwenyekiti wa mtaa wa misheni na afisa afya wa kata hiyo  juu suala hilo lakini   wamelikalia kimya jambo hilo.

Sauti ya balozi wa eneo  Samwel Lubinza Fimbo 

Mwenyekiti wa mtaa wa misheni Joseph Protas ameshangazwa na kitendo cha Serikali ya wilaya  kumwaga taka karibu na makazi ya watu  huku  akimuomba  afisa mazingira wa  Halmashauri ya Sengerema kuondoa taka hizo  katika eneo hilo .   

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa misheni Joseph Protas

Naye afisa Mazingira  wa Halmahsuri ya wilaya ya Sengerema  Tandi Laiza  amewaomba radhi wananachi kwa kitendo hicho na kuahidi  kulifanyia kazi  suala hilo.

Sauti ya afisa Mazingira  wa Halmahsuri ya wilaya ya Sengerema  Tandi Laiza