Sengerema FM

Mkurugenzi Sengerema aanza kutekeleza Agizo la Paul Makonda

14 November 2023, 8:54 am

Viongozi wa Halmashauri ya Sengerema wakikagua eneo la Stendi ya Mwembe yanga iliyopo mjini Sengerema. Picha na Joyce Rollingstone

Stendi ya Mwembe yanga ilikuwa msaada mkubwa kwa wananchi kutoka halmashauri ya Buchosa na Geita vijijini kwani hapo awali walikuwa wakiitumia stendi hiyo wanapokuja mjini Sengerema jambo ambalo liligeuka na kuleta changamoto kwa takribani mwaka mmoja baada ya kufunguliwa kwa stendi mpya ya Bukala ambapo ilipelekea stedi hiyo kufungwa, Wananchi wamekua wakilipigia kelele wakiomba kurejeshwa kwa stedi hiyo na mnamo nov12 Katibu wa itikadi na uenezi CCM Paul Makonda alimuangiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Sengerema kuifungua Stendi hiyo mara moja..

Madereva wa magari pamoja na wafanyabiashara wa stendi ya mwembe yanga wilayani sengerema mkoani mwanza, wametakiwa kufuata sheria na taratibu ikiwa ni pamoja na kulipia ushuru wa standi ili kuepuka usumbufu.

Hayo yamebainishwa na kaimu mkurugenzi wa halimashauli ya wilaya ya sengerema ndugu MWITA WARYUBA,katiak zoezi la ufunguzi wa standi ya mwembe yanga nakusema kuwa kuanzia leo Novemba 14 mwaka huu  magari yote ya yanayotoka halmashauri ya Buchosa yanaanza rasmi kuingfia ndani ya stendi hiyo.

Naye mh,diwani wa kata ya nyampulukano Bwn.AMRI KAHOGO amesema zoezi la ugawaji wa maeneo ya biashara katika eneo hilo litaafanyika hivyo wenye uhitaji wa maeneo wannatakiwa kufika kwa ajili ya zoezi la ugwaji maeneo.

Hata hivyo ufunguzi wa stendi hiyo umejiri kufuatia agizo lililotolewa na Katibu wa itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Paul Makonda novemba 12 mwaka huu wakati akiwahutubia wanchi Wilayani Sengerema.

Taarifa ya Joyce Rollingstone inafafanua zaidi