Sengerema FM

Wananchi walia kutelekezwa eneo la stend Sengerema

1 November 2023, 5:20 pm

Eneo ilipokuwa stend ya Mwembeyanga iliyokuwa ikitumika na magari Madogo ya Sengerema -Buchosa likiwa wazi tangu mwezi March 2023. Picha na Emmanuel Twimanye

Ikumbukwe kuwa kwenye mkutano wa Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh. Senyi Ngaga uliofanyika katika eneo la ujenzi wa shule ya sekondari Nyampulukano mwezi Mei mwaka huu ,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema Binuru Shekidele aliwaahidi wananachi kuwa stendi hiyo itarejeshwa  mwezi Julai mwaka huu ambapo mpaka sasa hakuna kinachoendelea kwenye eneo hilo.

Na:Emmanuel Twimanye.

Wananchi mtaa wa Mnadani kata ya Nyampulukano Sengerema mkoani Mwanza wamemlalamikia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Binuru Shekidele kwa madai ya kuchelewa kutekeleza ahadi ya kurejesha stendi ya magari madogo  ya Mwembeyanga.

Wakizungumza na Radio Sengerema  baadhi ya wananachi katika eneo la stendi hiyo wamesema kuwa licha ya Mkurugenzi mtendaji  kuwaahidi  kuirejesha stendi hiyo mwezi Julai mwaka huu lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji wowote .

Katibu wa Mwenyekiti wa mtaa wa Mnadani  Peter Ndimila amekiri kutorejeshwa kwa stendi hiyo hadi sasa na kuiomba serikali kufanya haraka mchakato wa kuirejesha ili  kuchochea uchumi wa wanachi wa eneo hilo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele amesema kuwa wanasubiri kukaa kikao kwa ajili ya kupata hatima ya stendi hiyo.

Taarifa ya Emmanuel Twimanye inafafanua zaidi.