Sengerema FM

Waganga wa tiba asili Sengerema waonywa kuacha kuwatapeli wateja wao

12 May 2026, 7:08 pm

Mwenyekiti wa Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Wilaya ya Sengerema, Juzaki Juzaki akizungumza na waganga, Picha na Emmanuel Twimanye

Baada ya kuibuka kwa tabai za baadhi ya wataalamu wa tiba asili kuwatapeli wateja wao Mwenyekiti wa Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Sengerema atoa onyo dhidi yao wanaojipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Na,Emmanuel Twimanye

Waganga na wakunga wa tiba asili Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuacha tabia ya kutoa masharti magumu kwa wateja wanaofika katika maeneo yao kwa ajili ya kupata huduma za matibabu, kwa lengo la kuwatapeli fedha zao.

Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Wilaya ya Sengerema, Juzaki Juzaki, kufuatia kuwepo kwa baadhi ya waganga wanaodaiwa kutumia njia hiyo ili  kuwatapeli  wananchi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Wilaya ya Sengerema, Juzaki Juzaki

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo  amewahakikishia wananchi kuwa waganga matapeli watachukulia hatua za kisheria ili kudhibiti suala hilo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Wilaya ya Sengerema, Juzaki Juzaki

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi   wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria waganga matapeli,ili  kukomesha tabia hiyo.

Sauti za baadhi ya wananchi