Sengerema FM

Mwanamke akutwa amefariki kitandani kwake

9 January 2024, 8:43 am

Wananchi na majirani wakisikitika baada ya kukuta mpendwa wao amefariki Dunia ndani kwake.Picha na Emmanuel Twimanye

Matukio ya watu kukutwa wamefariki Dunia yanazidi kushika kasi wilayani Sengerema ambapo baadhi yao wanadai yanasababishwa na msongo wa mawazo pamoja na ugumu wa maisha kwa watu jambo lililopelekea mwenyekiti wa mtaa wa Migombani wilayani hapo kuwataka wananchi kuwa na tabia ya kujuliana hali asbuhi kila siku kabla ya kwenda kwenye majukumu yao.

Na:Emmanuel Twimanye.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 41 amekutwa akiwa amefariki kitandani katika mtaa wa migombani kata ya Nyampulukano Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza huku chanzo cha tukio hilo kikiwa hakijafahamika.

Mashuhuda  ,mmiliki wa nyumba  na majirani  wamesema kuwa wamebaini tukio hilo baada ya kijana mmoja anayefanya kazi na mme wa marehemu Simon Mathias  kufika  nyumbani hapo majira ya saa mbili na nusu asububi  akimtafuta na kwamba   walipobisha hodi katika chumba chake ilisikika sauti ya mtoto akimwita mama yake ndipo walipolazimika kuingia ndani na kukuta mwanamke huyo yuko kitandani akiwa amefariki Dunia.

Balozi wa eneo hilo  Peragia  Tete  amesema kuwa taarifa za tukio hilo amezipata kutoka kwa  mmiliki wa nyumba aliyokuwa amepanga mwanamke huyo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Migombani  Anton Busumabu  amethibitisha  kutokea kwa tukio hilo na kutaja jina la mwanamke aliye kutwa akiwa amefariki Dunia kuwa ni  Martina  Patrick Misalaba huku akiwataka   wananachi kujenga tabia ya kujuliana hali hususani nyakati za asubuhi.

Jeshi la Polisi Wilayani Sengerema limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kisha kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Taarifa ya Emmanuel Twimanye ikifafanua zaidi