Sengerema FM

TAKUKURU yawaburuza mahakamani watumishi 16 Sengerema

6 June 2024, 8:49 am

Baadhi ya watumishi wakiwa katika ukumbi wa mahakama ya Sengerema.Picha na Emmanuel Twimanye

Takukuru imezidi kutoa wito kwa wananchi mkoa wa Mwanza kusimamia Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Maeneo yao, Pamoja na kuzuia, kukemea vitendo vya rushwa katika Maeneo ya  kupata huduma

Na:Emmanuel Twimanye

Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani  Mwanza imewafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Sengerema   watumishi 16 wa Halmashauri ya Sengerema  kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha Zaidi ya Shilingi Zaidi ya milioni 87 zilizotokana na mapato ya ndani.

Akisoma mashtaka  yanayowakabili Mwanasheria mwandamizi wa Tasisis ya kuzuia na kupambana na Rushwa  Mkoani Mwanza  Moses   Malewo   mbele ya Hakimu Mwandamizi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Sengerema Evoid Augen Kisoka amesema kuwa  watumishi hao wote wanakabiliwa  mashtaka mbalimbali yakiwemo mashtaka ya matumizi mabaya ya Mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kupambana na Rushwa na kifungu cha 28  cha  ufujaji na ubadhilifu.

Hata hivyo  washitakiwa   hao  wote  baada ya  kusomewa mashtaka yao  wameachiwa kwa dhamana ambapo baadhi watafikishwa tena mahakamani hapo  June 19 na   wengine   June 25  mwaka huu.

Baada ya kusoma mashtaka hayo Mwanasheria mwandamizi wa Tasisisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa  Mkoani Mwanza  Moses   Malewo akiwa nje ya viunga vya mahakama amezungumza na waandishi wa habari na kuwatahadharisha watumishi wa Halmshauri  kuzingatia sheria kanuni na sheria zinazowaongoza katika ukusanyaji wa mapato na  kutojihusisha na vitendo vya rushwa . 

Sauti ya mwanasheria mwandamizi wa TAKUKURU  mkoa wa Mwanza  Moses   Malewo akizungumzia watuhumiwa wa ubadhilifu wa fedha zaidi ya mil.87 Sengerema

Nao baadhi ya wananachi Wilayani Sengerema  wameipongeza Takukuru kwa kuwafikisha mahakamani watumishi hao huku wakiomba kuchukuliwa hatua kali za kisheria  kwa wale watakaobainika kujihusisha na ubadhilifu huo wa fedha kwa kuwa wanachangia kurudisha nyuma maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.