Sengerema FM

Akatwa mapanga usiku akienda kwenye mkesha wa pasaka

2 April 2024, 3:13 pm

Mariam Sebagi mkazi wa  mtaa wa Misheni akiendelea na matibabu katika Hospitali Teule ya wilaya ya Sengerema. Picha na Emmanuel Twimanye

Mtu asiyejulikana amemjeruhi kwa mapanga mwanamke anayejulikana kwa majina ya Mariam Sebagi  mkazi wa  mtaa wa Misheni usiku akiwa na wenzake wakielekea kwenye mkesha wa Pasaka mjini Sengerema.

Na:Emmanuel Twimanye

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mariam Sebagi mkazi wa  mtaa wa Misheni wilayani Sengerema mkoani Mwanza amedaiwa kushambuliwa kwa mapanga na mtu  asiyejulikana  na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake, huku chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijafahamika .

Akizungumzia tukio hilo  mwanamke  huyo  akiwa amelazwa katika Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema  amesema kuwa wakati  anakwenda kwenye mkesha wa pasaka na wenzake  ndipo alitokea ghafla mtu  asiyejulikana   na kuanza kumshambulia kwa mapanga  sehemu mbalimbali za mwili wake

Sauti ya Mariam Sebagi    Mkazi wa  mtaa wa misheni, aliyejeruhiwa na panga Sengerema

Baadhi ya ndugu na majirani wa familia hiyo wamesikitishwa na kulaani vikali tukio hilo huku wakiiomba serikali kufanya uchaguzi wa tukio hilo ili kubaini  mtu aliyefanya kitendo hicho cha kinyama na kumchukulia hatua kali za kisheria.

Sauti ya Baadhi ya Majirani na Ndugu wa Mariam Sebagi wakizungumzia tukio hilo

Nesi muuguzi katika Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema Tabu  Makelemo  amekiri  kumpokea mwanamke huyo katika Hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu huku akiwa amepoteza fahamu   ambapo   kwa sasa hali yake inaendelea vizuri. 

Sauti Muuguzi katika Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema Tabu  Makelemo

Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Misheni Joseph Protas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  na kuahidi kushirikiana na jeshi la polisi kumtafuta mtu anayedaiwa  kutenda tukio hilo  .

Sauti ya mwenyekiti wa Mtaa wa Misheni Joseph Protas akithibitisha kutokea kwa tukio hilo

Hata hivyo Jeshi la polisi Wilayani Sengerema   limefika eneo la tukio  na  kushirikiana  na ndugu  kumbeba mwanamke huyo kisha kumpeleka katika   Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kupatiwa matibabu.