Sengerema FM

Yusuph Hodari akutwa amefariki uwanjani Sengerema

14 March 2024, 3:20 pm

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye eneo la tukio na mwili wa ndg. Yusuph Hodari uliokutwa eneo la mnadani Sengerema.Picha na Emmanuel Twimanye

Jeshi la polisi wilayani Sengerema limefika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu Yusuph Hodari aliyekutwa amefariki dunia eneo la Mnadani, kisha kuupeleka katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Na:Emmanuel Twimanye

Mtu mmoja amekutwa akiwa amefariki dunia katika mtaa wa Mnadani kata ya Nyampulukano wilayani Sengerema mkoani Mwanza, huku chanzo cha kifo hicho kikiwa bado hakijajulikana.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya ndugu na majirani wamesikitishwa na tukio hilo na kueleza kuwa  marehemu ameacha pengo kubwa katika familia na jamii kwa ujumla  kwa kuwa mchango wake ulikuwa bado unahitajika.

Sauti za ndugu na majirani wa marehemu Yusuph Hodari

Mwenyekiti wa kitongoji cha Mnadani Rajabu Mgala  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  na kutaja jina la kijana aliyefariki kuwa ni Yusuph Hodari, huku akiwashukuru wasamalia wema kwa kutoa taarifa baada ya kuona mwili huo.

Sauti Mwenyekiti wa kitongoji cha Mnadani Rajabu Mgala

Mwenyekiti wa mtaa wa kizugwangoma Kwiligwa methusela  amepokea taarifa  za tukio hilo  kwa masikitiko na kusema kuwa marehemu alikuwa ni Balozi katika mtaa wa Kizugwangoma huku akilipongeza jeshi la polisi wilayani Sengerema kwa kufika eneo la tukio kwa wakati.

Sauti Mwenyekiti wa mtaa wa kizugwangoma Kwiligwa methusela