Sengerema FM

Mkurugenzi aamuru wafanyabiashara kuondoka kando ya barabara

4 July 2023, 11:17 am

Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Sengerema Binur Mussa Shekidele akizungumza na wafanyabiashara. Picha na Elisha Magege

Kutokana na wafanyabiashara mjini Sengerema kuendesha shughuli zao pembezoni mwa barabara na kupelekea hofu ya kutokea ajali, hali hiyo imemuibua mkurugenzi wa halmashauri hiyo na kutoa siku tatu kwa wafanyabiashara hao kuondoka maeneo hayo .

Na: Said Mahera

Mkurugenzi Mtendaji wa  halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza ametoa siku 3 kwa wafanyabiashara wa matunda wanaouza pembezoni mwa barabara  mjini Sengerema kuondoka mara moja na kuhamia soko kuu kwa ajili ya kufanya biashara zao.

Mh  Binuru Shehkidele  amewataka wafanyabiashara kuondoka katika maeneo hayo kwani yanahatarisha  maisha yao.

Akizungumza na wafanyabiashara  hao baada ya kufanya ziara katika eneo wanaouza  matunda  mkurungenzi  wa halmashauri ya  Sengerema Mh. Binuru Shehkidele  amewataka wafanyabiashara kuondoka katika maeneo hayo   kwani yanahatarisha  maisha yao.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa matunda wamesema kuwa kuhamishwa katika sehemu hiyo na kupelekwa katika soko kuu itapelekea maisha yao kuwa  magumu kutokana na ugumu watakaoupata katika soko  hilo.

Hata hivyo mkurungezi huyo amewaomba viongozi wa wafanyabiashara wa matunda kama mjini Sengerema hawataridhika na sehemu hiyo wakae na wafanyabiashara hao na kupendekeza maeneo ambayo ni rafiki kwao lakini isiwe maeneo ya barabarani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa soko kuu  Bwn. Semeni Manoti amesema maeneo ya kufanyia biashara yapo  na kuwaomba wafanyabiashara wa matunda kuzingatia agizo la mkurungezi huku akiwaondoa wasiswasi muda wa kufunga soko hilo.

Suala la kuhamisha wafanyabiashara wa matunda katika maeneo ya pembezoni limekuwa likifanyika kila mara na wafanyabiashara hao kurudi katika maeneo hayo.

Sauti ya mwandishi Said Mahera akiripoti taarifa hii kuhusiana na wafanyabiashara mjini Sengerema.