Sengerema FM

Milioni 147 zatumika ukarabati wa madarasa shule ya msingi Sengerema

27 January 2024, 8:26 pm

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi.Senyi Ngaga akikata utepe kwenye uzinduzi wa madarasa 16 yalifanyiwa ukarabati na shirika la Support  School Fees Foundation. Picha na Emmanuel Twimanye

Shule ya Msingi Sengerema ni miongoni mwa shule kongwe nchini ambayo ilikuwa ikikabiliwa na uchakavu wa miundombinu hasa vyumba vya madarasa jambo lililopelekea wadau mbalimbali kujitokeza na kuanza kusaidia ukarabati.

Na;Emmanuel Twimanye.

Shirika lisilisolikuwa la Kiserikali  la  Suport  school  Fees Foundation kutoka nchini Uholanzi  limekarabati  majengo 16 katika shule ya msingi Sengerema  yenye thamani ya shilingi Milioni 147.

Mkuu wa wilaya Bi. Senyi Ngaga na viongozi wa halmashauri ya Sengerema wakikagua madara yaliyokarabatiwa katika shule ya Msingi Sengerema. picha na Emmanuel Twimanye

Akisoma taarifa ya ukarabati wa majengo hayo katibu wa shirika la Eco Faming Organisation Peter Mponeja  linalofanya kazi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo shirika la Suport school Fees amesema kuwa wamefanikiwa  kukarabati majengo 16 kati ya majengo 22 na kwamba majengo sita yaliyobaki yanatarajia kukarabatiwa muda sio mrefu.

Sauti ya katibu wa shirika la Eco Faming Organisation Bwn.Peter Mponeja

Mkurugenzi wa shirika la Suport School Fees Slyvian Mshjuis  amesema kuwa shirika hilo  lililenga kuwasaidia kuwalipia ada wanafunzi shuleni lakini  kwa sasa wamejikita kuwasaidia wanafunzi wengi  zaidi  .

Mkurugenzi wa shirika la Suport School Fees Bwn. Slyvian Mshjuis

Mkuu wa wilaya ya Sengerema aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa majengo hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makala amelipongeza shirika hilo kwa kukarabati majengo hayo ili kuwasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga

Awali akisoma taarifa ya shule ,Mwalimu Mkuu  wa shule ya Msingi Sengerema  Mwl,Samson  Mafuru  amesema kuwa baada ya ukarabati wa majengo hayo wanatarajia kuongezeka kwa mahudhurio ya wanafunzi kutoka  asilimia 90  hadi asilimia 100 pamoja na kuongezeka kwa  ufaulu wanafunzi katika mitihani ya ndani na taifa huku akilishukru shirika hilo kwa kuboresha shule hiyo.

Sauti ya Mwalimu Mkuu  wa shule ya Msingi Sengerema  Mwl,Samson  Mafuru