Sengerema FM

Watoto wawili wakamatwa kwa tuhuma za wizi Sengerema

15 May 2026, 8:01 pm

Watoto wanaotuhumiwa kujihusisha na wizi,Picha na Emmanuel Twimanye

Katika kukomesha tabia za baadhi ya watoto kujihusisha na vitendo vya wizi, wazazi na walezi Wilayani Sengerema wametakiwa kutoa malezi bora ili kuepuka  kujihusisha na vitendo hivyo vinavyoweza  kuhatarisha maisha yao.

Na, Emmanuel Twimanye

Watoto wawili wenye umri wa miaka 12 na 16 wamekamatwa katika mtaa wa Igogo Kata ya Nyampulukano Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kwa tuhuma za wizi wa vitu mbalimbali .

Wakizungumzia tukio hilo wakiwa chini wa ulinzi wa polisi jamii watoto hao wamekiri kuiba vitu mbalimbali na kueleza kuwa hiyo ni mara yao ya pili.

Sauti za watoto wanaotuhumiwa kuiba.

Mwanamke aliyebiwa vitu hivyo Elizabeth  Gidion  amesema watoto hao waliruka  ukuta  kisha kuingia ndani na  kuiba dish linalokadiliwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi  laki  tatu.

Sauti ya mwanamke aliyeibiwa Bi.Elizabeth  Gidion

Wazazi wa watoto hao wamesikitishwa na watoto wao kujihusisha na vitendo vya wizi na kuiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria ili liwe fundisho kwa watu weengine wenye tabia hiyo.

Sauti za wazazi wa watoto

Kamanda wa polisi jamii kata ya Nyampulukano Lenatus Lugadija amethibitisha kukamatwa kwa watoto hao kwa tuhuma za wizi na kuwaonya vijana kuachana na vitendo vya wizi.

Sauti ya Kamanda wa polisi jamii kata ya Nyampulukano Lenatus Lugadija.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa Igogo Goodluck Daud  amewataka wazazi kuwa makini na malezi ya watoto wao watoto ili kuepuka  kujihusisha na vitendo hivyo vinavyoweza  kuhatarisha maisha yao.

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Igogo Goodluck Daud.