Sengerema FM

CCM yazindua kampeni za udiwani Sengerema

11 March 2024, 6:03 pm

Wanachama wa chama cha mapinduzi CCM Wakicheza ngoma za kisukuma wakati wa uzinduzi wa kampeni kata ya Buzilasoga.Picha na Emmanuel Twimanye

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 23 Tanzania Bara, ukitarajiwa kufanyika tar 20 Machi 2024 Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima, R. K jijini Dodoma tar15 Februari, 2024 miongoni mwa kata zilizotangazwa kufanya uchaguzi huo ni kata ya Buzilasoga iliyopo Halmashauri ya Sengerema.

Na:Emmanuel Twimanye.

Chama cha Mapinduzi (CCM ) Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Buzilasoga Wilayani Sengerema   ili  kuziba  nafasi   ya kiti hicho  kilichoachwa wazi  baada ya  Diwani aliyekuwepo David  Shilinde  kufariki Dunia mwezi Septemba 28 2023.   

Mbunge wa jimbo la Sengerema Mh. Hamis Tabasam akizungumza na wananchi wa kata ya Buzilasonga kwenye uzinguzi wa kampeni za udiwani. Picha na Emmanuel Twimanye

 

Akizindua kampeni hizo mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema Mark Agustine Makoye amewataka wananchi  kuchagua  kiongozi bora atakayewaletea maendeleo na si vinginevyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Sengerema Mark Agustine Makoye akifungua kampeni za chama hicho kata ya Buzilasoga

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam amemuomba mgombea udiwani kata ya Buzilasoga  kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Edina Godwin Bandihai  endapo akichaguliwa  kuwa diwani wa kata hiyo kuhakikisha  anatatua kero za wananchi ikiwemo  uhaba wa maji .

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam akimnadi mgombea wa udiwani kupitia ccm kata ya Buzilasoga

Naye mgombea udiwani kata ya Buzilasoga kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi ( CCM)  Edina  Godwin Bandihai  ameahidi kutatua kero za wananchi pindi atakapochaguliwa.  

Sauti ya Bi.Edina  Godwin Bandihai  Mgombea udiwani kata ya Buzilasoga

Aidha  Jumla ya  wagombea   nane wa  vya siasa  wanachuana katika kinyang’anyiro cha   udiwani kata ya Buzilasoga  katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa  kufanyika   Machi, 20 mwaka  2024.
Wagombea waliopo katika kinyanganyiro hicho   ni pamoja na Edina Godwin Bandihai (CCM), Deus Kabilondo Nkwabi (NLD), Mhoja Mathias Lubinza (ADC), Ramadhan Omary Said (UPDP), Saida Ramadhan Abdul (SAU), Rehema Hussein Khery (AAFP), Anna Sulwa Zengo (CCK) na Msafiri Joseph Nyamwitanga (Demokrasia Makini).