Sengerema FM
Sengerema FM
4 May 2026, 12:09 pm

Jeshi la zima moto Sengerema latoa elimu kwa wanchi kuhusiana na matumizi sahihi ya namba za kutoa taarifa za dharula kwa jeshi hilo
Na:Emmanuel Twimanye
Wananchi Wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameonywa kuacha kuchezea namba za dharura za Jeshi la Zimamoto na kutoa taarifa za uongo za matukio ya moto.
Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa Jeshi la zima moto na uokoaji wilayani Sengerema, Inspekta Juma Ngwembe,wakati akitoa elimu ya kukabilianan na majanga ya moto kwa wananachi kuelekea maadhimisho ya siku ya zimamoto Dunia na kusema kuwa vitendo hivyo vinakwamisha juhudi za uokoaji na vinaweza kuhatarisha maisha ,
Askari wa Jeshi la zima moto na uokoaji Wilayani humo Konstebo Erick Karumuna amesema changamoto kubwa wanazokumbana nazo ni kupokea simu za uongo,pamoja na kuchezewa simu ya dharura hali inayorudisha nyuma mapambano dhidi ya majanga ya moto.
Baadhi ya wananchi wameliomba jeshi hilo kuachukulia hatua kali za kisheria watu wanaochezea simu ya dharura pamoja na kutoa taarifa za uongo za majanga ya moto ili kukomesha tabia hiyo.
Aidha maadhimisho ya siku ya Zima moto Duniani yanafanyika Mei 4 mwaka huu kwa lengo la kuwaheshimu na kuwakumbuka waliopoteza misha wakiwa kazini ,kuthamini mchango wao katika kuokoa maisha na kutoa elimu kwa jamii kuhusu usalama wa moto.