Sengerema FM

Fisi wavunja mlango, watokomea na mbuzi saba wa familia moja Sengerema

5 December 2023, 6:56 pm

Bi. Coletha Mapambano akionyesha namna fisi walivyo vunja mlango na kutokomea na mbuzi saba usiku.Picha na Emmanuel Twimanye

Matukio ya fisi kushambulia mifugo na binadamu yameendelea kushika kasi wilayani Sengerema licha ya jitihada za serikali  na mamlaka za wanyamapori kukabiliana na wanyama hao lakini bado fisi na mamba imekuwa tishio.

Na:Emmanuel Twimanye

Kundi la fisi limevamia kwa mkazi mmoja wa kitongoji cha Magutu kijiji cha Ibondo kata ya Ibondo wilayani Sengerema mkoani Mwanza  na kushambulia mbuzi saba kisha kutokomea nao kusikojulikana hali iliyozua taharuki kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Akizungumzia tukio hilo mmiliki wa mbuzi hao Coletha Mapambano amesema kuwa aliamka majira ya saa tisa usiku kwa ajili ya kuwapeleka watoto kujisaidia na kukuta hali hiyo na kwamba hali hiyo imemrudisha nyuma kimaendeleo.

Baadhi ya majirani na wananachi wameshangazwa na kusikitishwa na tukio hilo huku wakilihusisha na masuala ya imani za kishirikina .

Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Magutu Mgwesa Joseph amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka  wafugaji kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama hao.

Taarifa ya Mwandishi wetu Emmanuel Inafafanua zaidi