Sengerema FM

Fisi Maria14 avuruga kikao cha madiwani Sengerema

3 March 2024, 6:58 pm

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga wa pili kushoto akitolea ufafanuzi suala la Fisi kuwa tishio Chifunfu.Picha na Emmanuel Twimanye

Kufuatia kuwepo kwa changamoto ya wanyama fisi katika kata ya Chifunfu iliyopo Halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza Diwani wa kata hiyo Robert Madaha amelifikisha jambo hili kwenye kikao cha Baraza la Madiwani ambapo limeibua hisia mpya baada ya kuonekana baadhi ya fisi wana majina, shanga na namba za usajili.

Na;Emmanuel Twimanye

Fisi sita akiwemo aliyekuwa ameandikwa jina la Maria namba  14 akiwa amevaa heleni na wengine waliokuwa wamevaa shanga  wameuawa na wataalam wa jadi katika kijiji cha Chifunfu kata ya Chifunfu wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata ya Chinfunfu  Madaha katika mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmahauri ya Wilaya ya Sengerema na kusema kuwa fisi na mamba  wamekuwa tishio katika kata hiyo na kuiomba serikali kuingilia kati suala hilo.

Sauti ya Diwani wa kata ya Chifunfu Mh. Robert Madaha

Baadhi ya wananchi wameshangazwa na tukio hilo na kuiomba jamii kumrudia Mwenyezi Mungu .

Sauti za Wananchi Wilayani Sengerema

Kufuatia hatua hiyo  Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Ngaga amemuomba Diwani  wa kata ya Chifunfu kukaa na wazee ili kulitafutia ufumbuzi suala hilo huku akiwaomba wananachi kuwa makini dhidi ya wanayama hao.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi.Senyi Ngaga

Aidha matukio ya fisi na mamba yameendelea kushika kasi wilayani Sengerema  na kupelekea vifo kwa binadamu huku wengine wakiachwa na ulemavu licha ya serikali kuendelea kukabiliana na  wanyama hao.