Sengerema FM
Sengerema FM
9 June 2026, 7:49 pm

Wazazi na tasisi za kidini waiomba serikali kuingilia kati suala la mmomonyoko wa maadili kwa vijana katika jamii.
Na, Emmanuel Twimanye
NSerikali imeombwa kuingilia kati suala la baadhi ya mabinti wanaovaa mavazi yasiyo na staha kwa kuweka sheria na miongozo ya kudhibiti suala hilo ili kulinda maadili ya Kitanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa taasisi ya ELGIBO Edina Ezekiel Lyanga inayojishugulisha na huduma ya maombi na maombezi kwa watu wenye mahitaji wilayani Sengerema, wakati akizungumzia tatizo la mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Amesema serikali ina uwezo wa kudhibiti suala la mavazi yasiyo na staha katika jamii kama ilivyofanikiwa kuweka utaratibu wa wanafunzi kuvaa mavazi yenye staha shuleni, hatua ambayo imechangia kudumisha nidhamu na maadili shuleni.
Katika hatua nyingine katibu huyo, amewakumbusha wazazi na walezi umuhimu wa kuwalea watoto katika maadili mema ili kukabiliana na tatizo la mmomonyoko wa maadili ambalo limeendelea kushika kasi katika jamii na kuathiri kizazi cha sasa na kijacho.
Kwa upande wao, baadhi ya wazazi na walezi wamekiri kuwepo kwa tatizo la mmomonyoko wa maadili miongoni mwa watoto, huku wakiahidi kushirikiana katika kuimarisha malezi na kuwalea watoto katika maadili mema ili kujenga jamii yenye nidhamu na maadili bora.