Sengerema FM
Sengerema FM
6 August 2026, 10:02 am

Jeshi la polisi wilaya ya Sengerema kutoa taarifa za matukio ya uvunjifu wa amani hasa matukio ya ukatili dhiidi ya watoto katika jamii
Na,Elisha Magege
Jeshi la polisi wilaya ya Sengerema limeendelea kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia huku likiwataka wananchi kutoa taarifa za uvunjifu wa Amani na uwepo wa matukio ya kihalifu katika jamii.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Buyagu Polisi kata wa kata hiyo Inspt. Alex Joseph Mtwangi amesema jeshi la polisi limeamua kufika maeneo yote yenye mikusanyiko kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kutoa taarifa pindi matukio ya uvunjifu wa Amani yanapotokea katika jamii.
Kwa upande wake Inspt. Mayeji Busumabu amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuacha kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa ili waweze kutimiza malengo yao.
Naye mkuu wa Shule ya Sekondari Buyagu Mwl. Aurelian Sandi amelishukuru Jeshi la polisi kwa kufika shuleni hapo na kutoa elimu hiyo huku akilisihi jeshi hilo kufika mala kwa mala kutoa elimu ya masuala ya ukatili na kutunza Amani ya nchi hasa kwa vijana.
Aidha jeshi la polisi wilayani Sengerema limewataka wananchi kuilinda Amani iliyopo na kufanya kazi ili kujiingizia kipato.