Sengerema FM

Mme amkata mapanga akitaka warudiane

4 January 2024, 3:40 pm

Mwanamke aliye jeruhiwa kwa panga na mtu anaye dhaniwa kuwa mme wake kwa madai ya kugoma kurudiana nae.Picha na Emmanuel Twimanye

Imekuwepo tabia ya baadhi ya wanandoa wanapo tarakiana, mmoja wao kushindwa kukubaliana na hali jambo hili limepelekea baadhi ya kuchukua maamzi ya kujitoa uhai au kutoa uhai wa wenzi wao wa zamani wakihisi itasaidia ndio sababu iliyomkuta Bwana Masolwa Maliki baada ya kumtaka mkewe warudia kwa takribani mwaka mmoja sasa huku yeye akikataa.

Na:Emmanuel Twimanye.

Mwanamke mmoja katika kitongoji cha Isungang’holo kata ya Nyatukala Wilayani Sengerema amedaiwa kuvamiwa na mwanaume aliyekuwa mme wake kisha kushambuliwa kwa mapanga na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa madai ya kukataa kurudiana naye.

Akizungumzia tukio hilo mwanamke huyo akiwa amelazwa katika Hospitali teule ya wilaya ya Sengerema amesema kuwa alivamiwa na mwanaume huyo majira ya saa mbili usiku kisha kuanza kumshambulia kwa mapanga kichwani na mikononi.

Ndugu na baadhi ya wananchi wamesikitishwa na tukio hilo na kuiomba serikali kumtafuta mwaname huyo na kumchukulia hatua kali za kisheria.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isungang’holo Marco sumuni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa wanaendelea kumtafuta mwaname huyo ili waweze kumfikisha kwenye mikono ya sheria.

Naye mratibu wa Dawati la jinsia na watoto kutoka jeshi la polisi wilayani Sengerema Mponela Malongo amelaani vikali tukio hilo na kuahidi kulifuatilia ili kuhakikisha mtuhumiwa huyo anakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Taarifa ya Emmanuel Twimanye inafafanua zaidi