Sengerema FM
Sengerema FM
12 May 2026, 6:18 pm

Kufuatia kukithili kwa watu kujichukulia sheria mkono Jeshila Polisi Mwanza lawakamata watu tisa kwa mauaji.
Na, Emmanuel Twimanye
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu tisa wakiwemo Mabaunsa wa baa ya Rasvegas kwa tuhuma za mauwaji ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mzafaru Faizar (26) mkazi wa Kata ya Mbugani Jijini Mwanza kwa kushindwa kulipa bili ya shilingi elfu nane baada ya kunywa pombe.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mtafungwa amethibitisha kutokea tukio hilo.
Kamanda Mtafungwa, amebainisha kuwa baada ya kufanyika kwa tukio hilo jeshi la polisi lilianza kufanya upelelelezi na kufanikiwa kuwakamata baadhi ya watuhumiwa wa mauaji hayo.
Aidha, Kamanda Mtafungwa amewataka walinzi wa baa na maeneo ya starehe kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, na badala yake kuwafikisha watuhumiwa kwenye vyombo vya dola ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.