Sengerema FM

Zaidi ya watoto 100,000 Sengerema kupatiwa matone ya vitamini A

2 December 2023, 11:14 am

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema Bi.Yusta Mwambembe akimpatia matone mtoto kwenye ufunguzi wa matone wa vitamini A. Picha na Deborah Maisa

Halmashauri ya Sengerema inatarajia kutoa matone ya Vitamin A pamoja na dawa za kutibu minyoo ya tumbo kwa watoto wasio pungua 100,285 wenye umri chini ya miaka 5 ambayo yameambatana na tathimini ya hali ya lishe.

Na;Deborah Maisa.

Zaidi ya watoto laki moja mia tatu na ishirini na nane wanatarajiwa kupatiwa matone ya vitamin A kwa ajili ya kuwakinga na magonjwa mbalimbali Wilayani Sengerema..

Akizungumza suala mganga mkuu wa halmashauri ya sengerema Dkt. Fedrick Mgalula kwenye uzinduzi wa chanjo ya matone  katika  kituo cha afya nyatukala amesema kwa wilaya nzima ya sengerema kuanzia disemba moja hadi Desemba 31 wanatakiwa kuwa wamewafikia watoto laki moja mia tatu ishirini na nane na kuwapa chanjo yamatone.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Yusta Mwambembe ambaye amemwakilisha mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema Binuru Shekidele amewataka akina mama kufuata utaratibu wanaopewa na madakitari ya kuwanyonyesha watoto na kutowaficha watoto wenye ulemavu.

Nao akina mama waliofika kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa chanjo ya matone wameishukuru serikali kwa kutoa kipaumbele kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano kupatiwa chanjo hiyo ambayo itawakinga na magonjwa mbalimbali.

Taarifa ya Deborah Maisa inafafanua zaidi