Sengerema FM

DC Sengerema ageuka mbongo murundikano wa uchafu mjini

23 January 2024, 9:42 pm

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh. Bi. Senyi Ngaga ameongozana na maafsa kukagua hali ya usafi katika soko kuu mjini Sengerema. Picha na Emmanuel Twimanye

Pamoja na kuwepo kwa taarifa za ugonjwa wa kipindupindu Nchini Madampo mjini Sengerema yanaonekana kujaa uchafu hali inayoleta wasiwasi kwa wananchi wakihofia kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo.

Na;Emmanuel Twimanye.

Wafanyabishara wa soko kuu mjini Sengerema wameilalamikia Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema kwa kuchelewa kuondoa taka zilizopo katika  dampo la soko hilo , hali inayohatarsisha   usalama wa afya zao katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Wametoa malalamiko hayo baada ya mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh.Senyi Ngaga kutembelea na  kukagua  hali ya usafi katika  soko hilo na kusema kuwa   taka  hizo    zimedumu kwa muda mrefu bila kuondolewa na wahusika licha ya wafanyabishara  kutoa tozo ya taka .

Sauti ya Wafanya biashara soko kuu mjini Sengerema

Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele ameahidi kuondoa taka hizo kwa wakati ili kuwaondolea kadhia hiyo.

Sauti ya Mkurugezi mtendaji Halmashauri ya Sengerema Binuru Mussa Shekidele

Naye Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Ngaga amemwagiza mkurugenzi mtendaji na afisa afya Wilbard Muyumbu kuhakikisha wanaondoa taka hizo kila siku na si vinginevyo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi Senyi Nganga