Sengerema FM

Wananchi Sengerema wajitokeza kuchukua vitambulisho vya NIDA

22 February 2024, 4:42 pm

Msimamizi wa zoezi la ugawaji vitambulisho kata ya Nyampulukano Bwn. Benedict Kamfune akiendelea kugawa vitambulisho kwa wananchi kata ya Nyampulukano.Picha na Emmanuel Twimanye

Wananachi wa Kata ya Nyampulukano Wilayani Sengerema  Mkoani Mwanza  Mwanza wamejitokeza kwa wingi kupata  vitambulisho ya Taifa (NIDA).

Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA Wilaya ya Sengerema imeanza zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya NIDA kwa wananchi,huku likiwataka kujitokeza kwa wingi ofsi za kata walizojiandikishia.

Na;Emmanuel Twimanye

Wakizungumzia zoezi hilo baadhi ya wananchi waliopatiwa vitambulisho hivyo wameishukuru serikali kwa kuleta vitambulisho  hivyo kwa kuwa vinamchango mkubwa katika kufanikisha maendeleo yao.

Sauti za Wananchi wakizungumzia namna zoezi lilivyokuwa la utoaji vitambulisho.

Naye msimamizi wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho  katika kata ya Nyampulukano  Benedict Kamfune  amesema  kuwa mwitikio wa wananchi kujitokeza kuchukua vitambulisho hivyo ni mkubwa huku akiwaomba wananchi kuendelea kujitokeza  kuchukua vitambulisho hivyo katika ofisi  ya Afisa mtendaji  wa kata.

Sauti ya Msimamizi wa zoezi la ugawaji vitambulisho kata ya Nyampulukano Bwn. Benedict Kamfune

Aidha zoezi la utoaji wa vitambulisho vya taifa (NIDA) bado linaendelea  katika vituo mbalimbali Wilayani Sengerema.