Sengerema FM

Inspector Mtwangi ahamasisha wananchi kuchangia damu Sengerema

31 July 2026, 4:49 pm

Polisi jamii kata ya Buyagu Inspector Alex Joseph Mtwangi na msafara wake ukizungumza na wanafunzi shule ya Sekondari Buyagu kuhusu kuchagia damu kwa hiari

Kutokana na kuwepo kwa vifo vinavyotokana na ukosefu wa damu salama katika Bank ya Damu hapa nchi wananchi wametakiwa kujitolea kwa hiari kuchangia ili kuokoa maisha ya wenye uhitaji.

Na,Elisha Magege

Jamii imehimizwa kujitokeza kuchangia Damu ili kusaidia kuokoa maisha ya wenye uhitaji Nchini.

Wito huo umetolewa na Polisi kata wa kata ya Buyagu Inspector Alex Joseph Mtwangi alipokuwa akizungumza na wanafunzi shule ya Sekondari Buyagu, ambapo amesema kuchangia damu ni kuokoa maisha yako na ya ndugu yako pale atakapo kuwa akihitaji.

Sauti ya Polisi jamii kata ya Buyagu Inspector Alex Joseph Mtwangi

Wakizungumzia faida za kuchangia Damu mganga mfawidhi Zahanati ya Buyagu Dr.Damas Dalama Na Dr Isdor Barnabas Mfawidhi katika Zahanati ya Isole Wamesema unapochangia Damu inasaidia mwili kutengeneza damu mpya.

Sauti za mganga mfawidhi Zahanati ya Buyagu Dr.Damas Dalama Na Dr Isdor Barnabas wa Zahanati ya Isole

Hata Hivyo mkuu wa Shule ya Sekondari Buyagu Mwl. Aurelian Sandi amelishukuru Jeshi la polisi kwa kufika shuleni hapo na kuhamasisha uchangiaji damu.

Sauti ya mkuu wa Shule ya Sekondari Buyagu Mwl. Aurelian Sandi

Nao baadhi ya Wanafunzi katika shule hiyo wamesema watakua mabalozi wa kuhamasisha jamii wakiwa shule na hata watakapo maliza masomo yao kuendelea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.

Sauti ya baadhi ya wananfunzi shule ya Sekondari Buyagu

Kwa mjibu wa tasisi ya mpango wa taifa wa damu salama (NBTS) imesema idadi ya wananchi kuchangia damu kwa hiari bado ni asilimia 60 kiwango ambacho hakitoshi kukidhi mahitaji nchini,hivyo haijitoshelezi na limeitaka jamii kujitokeza kuchangia kwa hiari.

Polisi jamii kata ya Buyagu Inspector Alex Joseph Mtwangi akizungumza na wanafunzi shule ya Sekondari Buyagu kuhusu kuchagia damu kwa hiari