Sengerema FM

Special Olypic 2026 yafana Sengerema

16 September 2026, 4:12 pm

Watoto wenye ulemavu wa akili wakifurahia kombe walilotwaa kwenye mashindano ya Special Olypic Sengerema.Picha na Elisha Magege

Wazazi na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu watakiwa kujua vipaji vya watoto wao mapema ili kuwasaidia kuondoa utegemezi.

Na;Elisha Magege

Jamii imetakiwa kuwapeleka shule watoto wenye mahitaji maalumu ili kuwasaidia kuchangamana na wenzao na kutambua vipaji vyao.

Rai hiyo imetolewa na Mwl. Kahabi Magessa afsa elimu kitengo maalumu msingi na awali katika Halmashauri ya Sengerema wakati akifungua mashindano ya michezo maalumu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu yaliyofanyika Shule ya msingi Sengerema, ambapo amesema mbali na haki yao ya k upata elimu bado watoto wenye mahitaji wanaweza kuwa na vipaji ambavyo kupitia walimu vinaweza kugundulika mapema.

Sauti ya Afsa elimu kitengo cha elimu maalumu Halmashauri ya Sengerema Mwl. Kahabi Magessa

Kwa upande wake mkurugenzi wa Shirika lisilo kuwa la kiserikali la AWPD Bwn.Sailence Nteko amesema watoto wanabadilika kulingana na mazingira hasa wanapochangamana na watoto wenzao.

Sauti ya mkurugenzi wa Shirika la AWPD Bwn.Sailence Nteko

Hata hivyo walimu  wakuu wa kitengo maalumu shule ya Msingi Sengerema na mkuu wa shule ya Msingi Busisi, wamesema jamii inapaswa kutambua kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wameboresha miundo mbinu ya kujifunzia kwa watoto wenye mahitaji maalumu nchini.

Sauti za walimu  wakuu wa kitengo maalumu shule ya Msingi Sengerema na mkuu wa shule ya Msingi Busisi

Nao baadhi ya wanafunzi wameishukuru serikali na wadauo shirika la AWPD kwa kuwakutanisha na kufanya michezo mbalimbali, huku wakiwataka wazazi na walezi kuwapeleka shule watoto wenye mahitaji maluumu.

Sauti ya baadhi ya wanafunzi wa shule za misingi Sengerema na Busisi

Mashindano ya Special Olpic 2026 yaliyozikutanisha shule za msingi vitengo maalumu Sengerema na Busisi yamefadhiliwa na shirika la AWPD.