Sengerema FM
Sengerema FM
4 May 2026, 12:31 pm

Changamoto za maisha zatajwa kuwa chanzo cha vijana kujinyonga wilayani Sengerema
Na:Emmanuel Twimanye
Kijana aliyefahamika kwa jina la Simeo Paschal (22) mkazi wa Mtaa wa Misheni Kata ya Misheni, wilayani Sengerema mkoani Mwanza amefariki dunia kwa kujinyonga ,huku chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijafahamika.
Baadhi ya ndugu wa marehemu pamoja na wakazi wa mtaa huo wamesikitishwa na tukio hilo na kuwaomba vijana kuepuka kuchukua maamuzi ya kujitoa uhai pindi wanapokumbana na changamoto za maisha.
Balozi wa eneo hilo,Safari Merikioli, amelaani vikali tukio hilo na kuwaomba vijana kuwashirikisha watu wa karibu pindi wanapokuwa na changaoti ili waweze kupatiwa ushauri .
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Misheni, Joseph Protas, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka vijana kuachana na tabia ya kujinyonga .
Jeshi la Polisi wilayani Sengerema limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu, kisha kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Sengerema kwa ajili ya taratibu za mazishi.