Sengerema FM

Afariki kwa kupigwa na radi-Sengerema

16 January 2024, 3:47 pm

Ramani ya kijiji cha Nyamasale kilichopo kata ya Busisi wilayani Sengerema: Picha msaada wa Googlemap

Baadhi ya watu wamekua na tabia ya kufanya kazi kwenye mvua, jambo ambalo linatajwa kuwa ni hatari sana, na katika halmashauri ya wilaya ya Sengerema mwanamke mmoja amefariki Dunia kwa kupigwa na radi akiwa shambani kuvuna mahindi wakati mvua ikiwa inanyesha.

Na:Emmanuel Twimanye

Mwanamke mwenye umri wa miaka 44 amefariki Dunia kwa kupigwa na Radi Katika Kijiji cha Nyamasale  Kata ya Busisi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.

Akizungumzia tukio hilo Edward Shigemelo kaka yake na marehemu amesema kuwa Dada yake  Roza Shigemelo alipigwa na radi na kupoteza maisha wakati akivuna mahindi shambani kwa ajili ya chakula cha familia.

Baadhi ya ndugu wa marehemu wamepokea tukio kwa masikitiko na kusema kuwa tukio hilo wamemwachia mwenyezi Mungu.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Nyamasale Shija Shinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwatahadharisha wananachi kuwa makini pindi mvua zinapokuwa zikinyesha.

Aidha  Jeshi la polisi Wilayani Sengerema  limewaruhusu ndugu wa marehemu kuendelea na taratibu za mazishi.   

Taarifa ya Mwandishi wetu Emmanuel Twimanye inafafanua zaidi