Sengerema FM
Sengerema FM
5 May 2026, 7:17 pm

Kufuatia kuwepo na malalamiko ya baadhi ya wamama kukimbia miji yao kama njia ya kukwepa kulipa madeni ya mikopo kutoka taasisi za kukopesha maarufu kausha damu, sasa washauriwa kuacha kukopa kwenye taasisi nyingi ili kuepuka fedheha ya kuacha watoto na waume zao.
Na;Emmanuel Twimanye
Wanawake wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameaswa kuacha kukopa mikopo kutoka taasisi za kiffedha zaidi ya moja ili kuepuka kukimbia familia kutokana na kushindwa kurejesha mikopo hiyo.
Ushauri huo umetolewa na afisa mikopo kutoka kampuni ya utoaji huduma za mikopo ya fedha ya JMS wilayani Sengerema, Neema Thomas, wakati akitoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi sahihi ya mikopo.
Bi. Neema amesema ni muhimu kwa wanawake wanaokopa fedha kuhakikisha wanazitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, ili ziweze kuwanufaisha kiuchumi na kuboresha maisha yao pamoja na familia zao.
Kwa upande wao,baadhi ya wanawake wakizungumza kwa nyakato tofauti wameshukuru kwa elimu hiyo kwa kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kuepuka kuchukua mikopo kutoka taasisi binafsi zaidi ya moja, jambo ambalo limekuwa likisababisha kushindwa kurejesha na kuathiri familia zao.