Sengerema FM

Mtoto afariki kwa kutumbukia kwenye shimo la choo mjini Sengerema

5 February 2024, 5:15 pm

Mwenyekiti wa Mtaa wa Geita road Bwn, Pelana Bagume akizungumza na majirani wa familia ya mtoto aliyefariki kwa kuzama kwenye shimo la maji. Picha na Tumain John

Wananchi mjini Sengerema wametakiwa kufunika au kufukia mashimo yaliowazi ili kuepusha matukio ya watoto kutumbukia na atakae kaidi sheria kali zitachukuliwa dhidi yake.

Na:Tumain John

Mtoto anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 5 mkazi wa mtaa Geita road kata ya Nyatukala wilayani Sengerema   anasadikiwa kufariki Dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo la choo.

Wakizungumza kwa maskitiko majira pamoja na mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa walipata taarifa kutoka kwa watoto waliokua wakicheza na marehemu huyo, kuwa ametumbukia kwenye shimo la choo lililokua limejaa maji ndipo wakaelekea eneo la tukio na kumkuta mtoto huyo tayari ameshafariki

Sauti ya majirani na mashuhuda wa tukio la mtoto kufa maji mjini Sengerema

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa Geita road  Bw Pelana Bagume amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja mtoto huyo kwa jina moja la martini ambae amefariki katika shimo hilo wakati akijalibu kutoa rigi la baiskeli alilokua akichezea na kutumbukia ndani ya shimo hilo.

Sauti ya Mwenyekiti mtaa wa Geita road Bw Pelana Bagume akizungumzia tukio la mtoto kufa maji mjini Sengerema

Hata hivyo jeshi la polisi Wilayani Sengerema limefika eneo la tukio na kuubeba mwili wa marehemu na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema,