Sengerema FM

Chama cha Mapinduzi cha shinda udiwani Kata ya Buzilasoga Sengerema

22 March 2024, 6:38 am

Msimamizi wa uchaguzi katika Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele akitangaza matokeo ya uchaguzi mdogo wa diwani kata ya Buzilasoga.Picha na Emmanuel Twimanye

Kata ya Buzilasoga ni miongoni mwa kata 22 za Tanzania bara ambazo tume ya uchaguzi ilitangaza kufanyika uchaguzi mdogo katika kata hizo ambapo mgombea wa chama cha mapinduzi ndiye aliyetangazwa kuibuka mshindi kati ya wagombea wengine nane kutoka vyama tofauti.

Na:Emmanuuel Twimanye

Mgombea udiwani   wa  chama cha Mapinduzi  (CCM) Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza Edina Godwin Bandihai    ameshinda  katika kinyang,anyiro cha uchaguzi mdogo  wa udiwani katika kata ya Buzilasoga  kwa kupata kura  5227 .

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa uchaguzi katika Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele  amemtangaza  mgombea udiwani wa chama cha mapinduzi CCM Edina Godwin Bandihai  kuwa  mshindi wa kiti cha udiwani katika kata  ya Buzilasoga  huku akifuatiwa na mpinzani wake Mhoja  Mathias Lubinza kutoka chama cha (ADC) aliyepata kura 242. 

Sauti ya Msimamizi wa uchaguzi katika Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele

Mgombea udiwani  aliyeshinda udiwani  kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Wilayani Sengerema Edina Godwin Bandihai  amewashukuru wapiga kura kwa kumchagua huku akiahidi kuwaletea maendeleao.

Sauti ya diwani mteule Kata ya Buzilasoga Bi. Edina Godwin Bandihai

Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Buzilasoga wamesema kuwa wanamatumaini makubwa na diwani huyo aliyechaguliwa huku wakimwomba kukamilisha ujenzi wa shule shikizi ya msingi kilabela pamoja na kukarabati miundombinu ya barabara.

Sauti za Wananchi wakazi wa kata ya Buzilasoga wakizungumzia uchaguzi wa udiwani katani hapo

Ikumbukwe kuwa wagombea waliokuwa wakichuana kuwania Kinyanganyiro cha   kiti cha udiwani katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Buzilasoga walikuwa ni pamoja na Edina Godwini Bandihai  (CCM) ambaye ameibuka mshindi ,Deus Kabilondo Nkwabi (NLD) ,Mhoja Mathias Lubinza (ADC)  Ramadhan Omary Said (UPDP) ,Said Ramadhan Abudul (SAU) Rehema Hussein Kheri (AAFP) ,Anna Sulwa Zengo (CCK) na Msafiri Joseph Nyamwitanga (Demokrasia makini.