Sengerema FM

RC Mwanza aipongeza Sengerema ujenzi wa madarasa.

16 January 2024, 4:48 pm

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makala akikagua vyumba vya madarasa na madawati katika shule ya msingi Pambalu iliyopo Sengerema mjini. Picha na Jovina George.

Mkuu wa mkoa wa mwanza Mh, Amos Mkala  baada ya kutamatisha ziara yake katika Halmshauri ya Sengerema,  ameendelea na ziara yake katika Halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema kwa ajili ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.

Na: Jovina George.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza   Mh, Amos Makala   amewapongeza viongozi wa chama na Serikali  Wilayani  Sengerema  kwa  kujenga  madarasa katika  shule ya msingi Pambalu.

Mh, Makala ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea katika shule hiyo na kukagua miundombinu ya vyumba vya madarasa na kukuta  zoezi la ujenzi linaendelea vizuri, huku akiunga mkono ujenzi huo kwa kutoa shilingi milioni tano.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema  Mark Augustine Mkaoye amesema kuwa shule hiyo inawanafunzi  wengi  hivyo  bado  inahitaji  vyumba vya madarasa  ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi .

Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Mh,Yanga Makaga amemhakikishia mkuu wa mkoa kuwa fedha zilizobaki kati ya milioni sabini zitakamilishwa na Halmshauri na kuanza ujenzi mara moja .

Awali akitoa taarifa ya shule  kwa Mkuu wa Mkoa  ,Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Pambalu Mwl. Sundi Mussa  amesema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa  madarasa 24  , madawati 183 na matundu  56 ya vyoo pamoja na ukosefu wa nyumba za walimu.

Taarifa ya Jovina George inafafanua Zaidi….