Sengerema FM

Mwizi wa kuku aua, atokomea kusikojulikana

5 February 2024, 5:04 pm

Wananchi wakiwa kwenye eneo la tukio la mauji yaliyotokea kijijini Nyamililo Sengerema. Picha na Emmanuel Twimanye.

Wananchi wataka sungusungu kurudishwa ili kukabiliana na vitendo vya uharifu pamoja na wizi wa kuku unaoendelea kutokea kata ya Sungamile Wilayani Sengerema.

Na:Emmanuel Twimanye

Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 40 ameuawa kwa kudaiwa kuchomwa na kisu na mtu anayedaiwa kuwa mwizi wa Kuku katika Kitongoji cha Bulunga B Kijiji cha Nyamililo kata ya Kasungamile Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.

Baadhi ya ndugu wa marehemu na wananchi wamesikitishwa na tukio hilo na kueleza kuwa marehemu Faustine masalu Mzigo wakati anatoka  kwenye disco vumbi  alikutana na mwizi huyo mtoni kisha kumuuliza amewatoa wapi kuku  hao ndipo  aliposhambuliwa kwa kisu na kupoteza maisha.   

Sauti za wananchi wakizungumzia tukio la mauaji lililotokea kijijini hapo.

Afisa mtendaji wa Kata ya Kasungamile Jenister Venance amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo  na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwabaini watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu katika kata hiyo.

Sauti ya Afisa mtendaji wa Kata ya Kasungamile Jenister Venance akithibitisha tukio hilo.

Naye Diwani wa kata ya Kasungamile  Mh,GodFrey Maisa amepokea tukio hilo kwa msikitiko na kuwaomba wananachi kutoogopa   kuwafichua watu wanaojihusisha na matukio hayo ya Kihalifu.

Sauti ya Diwani wa kata ya Kasungamile  Mh,GodFrey Maisa akizungumzia tukio hilo