Sengerema FM

Watoto wilayani Sengerema waiomba serikali kukomesha vitendo vya ukatili .

6 June 2026, 12:20 pm

Picha ya bango la maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika na baadhi ya watoto na wananchi walioshiriki madhimisho,Picha na Emmanuel Twimanye

Kutokana na kukithili kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto nchini, Afisa Tarafa ya Katunguru wilayani Sengerema Kibasa Samwel Masangwa ameitaka jamii kushirikiana na serikali ili kukomesha vitendo hivyo.

Na, Emmanuel Twimanye

Watoto Wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameiomba serikali kuchukua hatua madhubuti za kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto  ikiwa ni pamoja na  kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wa vitendo hivyo.

Hayo yamesemwa na watoto hao   katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kiwilaya katika Kata ya Nyamizeze Wilayani Sengerema  ambapo wamesema  vitendo vya ukatili bado vinaendelea katika baadhi ya maeneo na vinakwamisha haki zao za msingi.

Sauti za baadhi ya watoto wilayani Sengerema

Baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa wameahidi kuendelea kufichua matukio ya ukatili dhidi ya watoto ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Sauti za baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mh,  Senyi Ngaga, Afisa Tarafa ya Katunguru  Kibasa Samwel Masangwa  ameitaka jamii kushirikiana na serikali katika kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Sauti ya Afisa Tarafa ya Katunguru  wilayani SengeremaKibasa Samwel Masangwa

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Yuster Mwambembe ameahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Afisa Tarafa ya Katunguru ili kusaidia kukomesha vitendo hivyo.  

Sauti ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Yuster Mwambembe

Aidha, Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanatarajiwa kufanyika Juni 16 mwaka huu yakiwa na kaulimbiu isemayo, “Mtoto ni Malezi; Msingi wa Familia Bora kwa Taifa Imara.”

Picha ya bango la maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika na baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo, Picha na Emmanuel Twimanye
Baadhi ya viongozi walioshiriki maadhimisho hayo wakiwa katika picha ya pamoja ,Picha na Emmanuel Twimanye
Afisa Tarafa ya Katunguru wilayani Sengerema Kibasa Samwel Masangwa akihutubia washiriki wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, Picha na Eammanuel Twimanye