Sengerema FM

DC Ngaga akabidhi hati za kimila kupunguza migogoro ya ardhi Sengerema

8 May 2026, 6:23 pm

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga akikabidhi hati miliki ya kimila kwa mwananchi.Picha na Emmanuel Twimanye

Katika kukabiliana na migogoro ya ardhi Sengerema wananchi zaidi ya 1000 wakabidhiwa hati miliki za kimila

Na,Emmanuel Twimanye

Zaidi ya wananchi elfu moja katika Kijiji cha Ilekanilo, Kata ya Kasungamile, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, wamekabidhiwa hati miliki za kimila, hatua inayolenga kuimarisha umiliki wa ardhi na kupunguza migogoro.

Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa hati hizo, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mh, Senyi Ngaga, amesema hatua hiyo imekuwa suluhisho kwa migogoro ya ardhi, huku akiipongeza kampuni ya upimaji ardhi GMS kwa ushirikiano mzuri.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga,

Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema , Wilfred Mkono, amesema zoezi la upimaji lilianza Februari mwaka huu katika vijiji 16, na tayari vipande 18,639 vimepimwa huku hati 10,307 zikikamilika.

Sauti ya Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema Wilfred Mkono

Akizungumza kwa niaba ya wananachi waliokabidhiwa hati hizo Diwani wa Kata ya Kasungamile, Mh, Godfrey Maisa, ameishukuru serikali kwa kuwawezesha kumiliki ardhi zao kisheria.

Sauti ya Diwani wa kata ya Kasungamile Godfrey Maisa

Mkurugenzi wa GMS Geotech Consultancy  Company Limited, Michael Sambu, amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kushiriki zoezi hilo.

Sauti ya Mkurugenzi wa GMS Geotech Consultancy  Company Limited Michael Sambu
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga akikabidhi hati miliki ya kimila kwa mwananchi.Picha na Emmanuel Twimanye
Baadhi ya wananchi wakiwa katika foleni kuchukua hati miliki za kimila wilayani Sengerema