Sengerema FM

TCB Bank yawapiga msasa wasitaafu Sengerema

10 October 2023, 1:42 pm

Picha: Wazee wakipatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya pensheni. Picha na Anna Elias

Baadhi ya wastaafu wamekuwa na tabia ya kuoa vibinti vidogo baada ya kulipwa mafao yao jambo linalopelekea vifo vya mapema na kutoa laana kwa watoto wao nchini.

Na Anna Elias

Zaidi ya wastaafu 270 mjini Sengerema wamepatiwa mafunzo na benki ya TCB namna  ya kutumia pesheni zao pindi wanapomaliza muda wao wa  kazi.

Akitoa mafunzo hayo meneja msimamizi wa mikopo kwa wastaafu TCB Haika Mbaga kutoka Dar es Salaamu amesema wastaafu wana nafasi kubwa ya kujiendeleza kiuchumi na kuondokana na dhana ya kuwa maskini kwa kuzitambua fursa zinazowazunguka.

Amekemea baadhi ya wastaafu kuendekeza starehe kwa kunywa pombe na kuoa mabinti wadogo ambao malengo yao nikujipatia pesa hali inayochangia wastaafu kupoteza maisha kutokana na msongo wa mawazo.

Hata hivyo katika mafunzo hayo benk yaTCB imeandaa fursa kwa wastaafu kupata mikopo ya dharura ili kuwanusuru na mikopo ya kausha damu.

Kwa upande wao wastaafu wamepongeza benki ya TCB kwa Elimu hiyo huku wakiahidi kutumia pesheni zao kwa maendeleo yao na kuepuka mikopo umiza ambayo imekuwa mwiba kwa wastaafu.

Taarifa ya Anna Elias Inafafanua zaidi