Jukwaa la Mwanamke Sengerema lawashika mkono watoto wanaoshi mazingira hatarishi
3 March 2024, 7:29 pm
Kila mwaka ifikapo tar 08 Machi dunia huadhimisha siku ya mwanamke duniani ambapo hutanguliwa na matukio mbalimbali ambayo hufanywa na wanawake, Jukwaa la mwanamke Sengerema limeanza na kutoa msaada kwa wanafunzi wanaoishi mazingira hatarishi wilayani hapo.
Na;Emmanuel Twimanye
Zaidi ya wanafunzi 100 wanaoishi katika mazingira hatarishi katika shule ya msingi Ibondo wilayani Sengerema wamepatiwa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo madaftari.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya mwanawake duniani mwenyekiti wa jukwaa la Mwanawake wilayani Sengerema Bi.Darine Matonange amesema kuwa wanawake wilayani humo wameguswa kuwasaidia watoto hao ili wasome katika mazingira rafiki .
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ibondo Mwl,Paul Vicent amesema kuwa jumla ya wanafunzi 124 wanaoishi katika mazingira hatarishi wamepatiwa msaada huo .
Baadhi ya wanafunzi waliopatiwa msaada wamewashukuru jukwaa la mwanawake Sengerema kwa kutoa msada huo.
Naye kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Yuster Mwambembe amewataka wanawake kuendelea kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa na waume zao
Aidha siku ya Mwanawake Duniani ambayo hufanyika machi 8 kila mwaka, na Mwaka huu imebebwa na kauli mbiu isemayo “Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii”.