Sengerema FM

Walimu Sengerema wajikita kuchoma mkaa, kilimo badala ya kufundisha

22 January 2024, 6:40 pm

Jiwe la msingi la Shule ya Msingi Mayuya kilichopo Tabaruka. Picha na Emmanuel Twimanye

Shule ya msingi Mayuya ipo katika kata ya Tabaruka iliyopo Halmashauri ya Sengerema imekuwa ikifanya vibaya kwenye mitihani yake kutokana na changamoto ya Walimu wa shule hiyo kujikita katika shughuli zao binafsi za kuchoma mikaa na kilimo badala ya kufunsha.

Na;Emmanuel Twimanye.

Walimu wa shule ya Msingi Mayuya kata ya Tabaruka Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wamelalamikiwa  kwa madai ya kushindwa kufundisha  wanafunzi na kujikita katika shughuli za kilimo na uchomaji  mkaa.

Malalamiko hayo yameibuliwa na Mwenyekiti wa  Kitongoji cha Mtunduni  John Lubala Bushushu  katika kikao cha maendeleo ya kata na kusema kuwa walimu wamekuwa wakijikita zaidi katika shughuli za kilimo na uchomaji  mkaa  hali iliyopekekea  kushuka taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Sauti ya mwenyekiti wa  Kitongoji cha Mtunduni  John Lubala Bushushu

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mayuya Ladslaus Zacharia amesema kuwa shule hiyo haiwezi kupata matokeo mazuri kwa kuwa wanafunzi wamekuwa wakilazimika  kufanya mitihani sita ya kufunga muhula kwa siku moja kutokana na walimu kujikita katika shughuli zao binafsi.

Sauti ya mwenyekiti wa Kijiji cha Mayuya Ladslaus Zacharia

Akitolea ufafanuzi suala la wanafunzi kufanya mitihani sita kwa siku moja afisa elimu wa kata ya Tabaruka  Felister Nuge  amesema kuwa kwa utaratibu Mwanafunzi anatakiwa kufanya mitihani mitatu kwa siku.

Sauti ya Afisa elimu wa kata ya Tabaruka  Felister Nuge

Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mayuya  Mwl,Seleman Maige  ameahidi kuyafanyia kazi malalamiko hayo.  

Sauti ya mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mayuya  Mwl,Seleman Maige

Kufuatia hali hiyo Diwani wa kata ya Tabaruka Mh,Sospeter Busumabu amewaagiza afisa elimu wa kata hiyo Ferister Nuge ,afisa  mtendaji wa kata Sawia kimaro na afisa maendeleo   Philipo kamfune  kwenda  katika shule hiyo kufanya kikao  cha kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo.  

Sauti ya Diwani wa kata ya Tabaruka Mh,Sospeter Busumabu