Sengerema FM

Mwanamke auawa kwa kukatwa mapanga na wasio julikana Sengerema

19 February 2024, 8:13 pm

Baadhi ya ndugu wa marehemu waliofika nyumbani kwa Elizabeth Mang’ombe.Picha na Emmanuel Twimanye

Matukio ya watu kuawa kwa kukatwa mapanga yanazidi kukithiri wilayani Sengerema ambapo mpaka sasa tangu mwaka huu kuanza matukio matatu ya watu kuuawa kwa mapanga.

Na.Emmanuel Twimanye.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 40  Katika Kitongoji cha Nyakatome kata ya Kasungamile Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ameuawa kwa kukatwa na mapanga na watu wasiojulikana kwa  tuhuma za kujihusisha na Imani za kishirikina.

Bi. Nyabatiba Flano ambaye ni mama mzazi wa marehemu amesema kuwa  wakati wanakula chakula cha usiku waliona mwanga mkali wa tochi ukiwamulika na  baada ya  muda  mfupi walitokea  watu hao wasiojulikana kisha kuanza kumshambulia kwa mapanga  kichwani mtoto wake Elizabeth Mang’ombe na kupoteza maisha.

Sauti ya mama mzazi wa marehemu Bi. Nyabatiba Flano

Baadhi ya ndugu na majirani wamesikitishwa na tukio hilo na kuiomba serikali kufanya uchunguzi dhidi ya tukio hili ili kuwabaini watu walitekeleza mauaji hayo ya kinayama na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Sauti ya ndugu na majirani

Afisa mtendaji wa Kata ya Kasungamile  Jenister Venance amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwahakikishia wananachi kuwa watu waliotekeleza  tukio hilo watabainika. 

Sauti ya Afisa mtendaji wa Kata ya Kasungamile  Jenister Venance

Naye  Diwani wa kata ya Kasungamile  Mh, Godfrey  Maisa amelaani vikali tukio hilo na kuwataka viongozi wa serikali za vitongoji kunzisha polisi jamii katika maeneo yao ili kukabiliana na matukio hayo.

Sauti ya Diwani wa kata ya Kasungamile  Mh, Godfrey  Maisa

Jeshi la polisi Wilayani Sengerema limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kisha kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema.