Sengerema FM

Mama aomba binti yake achukuliwe hatua kali kwa wizi wa mahindi nyumbani

16 June 2026, 7:04 pm

Binti anayetuhumiwa kuiba mahindi akiwa chini ya ulinzi wa Polisi jamii, Picha na Emmanuel Twimanye

Baada ya baadhi ya watoto kuwa na tabia za wizi na udokozi wa vitu vya nyumabani, mama mmoja ameiomba serikali kumchukulia hatua za kisheria binti yake kwa wizi wa mahindi ili iwe fundisho kwa wengine.

Na, Emmanuel Twimanye

Binti aliyefahamika kwa jina la Sauda Selemani Mkazi wa mtaa wa Igogo Kata ya Nyampulukano Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mahindi.

Akizungumzia tukio hilo binti huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi jamii amekiri kuiba mahindi kiasi cha debe mbili na kwenda kuyauza.

Sauti ya binti anayetuhumiwa kuiba mahindi

Mama aliyeibiwa mahindi  ambaye pia ni mama mzazi wa binti huyo  Salah Isack amesikitishwa na tukio hilo  na kuiomba serikali kumchukulia hatua kali za kisheria binti huyo ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hiyo.

Sauti ya mama mzazi wa binti

Baadhi ya ndugu na majirani wamesikitishwa na kitendo cha binti huyo cha kujihusisha na wizi na kuwaomba mabinti kuachana na vitendo hivyo.

Sauti ya baadhi ya ndugu na marafiki wa mama mzazi wa binti

Kamanda wa polisi jamii kata ya Nyampulukano Lenatus Lugadija amethibitisha kukamatwa kwa binti huyo kwa tuhuma za wizi wa mahindi na kuahidi kumfikisha kwewnye vyombo vya dola kwa hatua zaidi za kisheria.

Sauti ya Kamanda wa Polisi jamii kata ya Nyampulukano Lenatus Lugadija

Kwa upande wake ,Mwenyekiti wa mtaa wa Igogo Goodluck Daud amewataka wazazi na walezi  kuwa makini na watoto ikiwa ni pamoja na kuwashauri  kuacha wizi  ili kuepuka kuhatarisha maisha yao.

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Igogo Goodluck Daud