Sengerema FM

CCM Sengerema yatatua mgogoro wa Ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 23

18 February 2024, 7:53 pm

Wajumbe wa kamati ya Sekretariet ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Sengerema wakizungumza na wananchi waliovamia eneo la shule ya msingi Kilabela Sengerema. Picha na Emmanuel Twimanye

Migogoro ya Ardhi wilayani Sengerema imekuwa Changamoto jambo lililoipelekea kamati ya Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi Sengerema kuanza kutembelea wananchi na kutatua ambapo imeanza na mgogo wa wananchi na Shule ya Msingi Kilabela uliodumu kwa zaidi ya miaka 23.

Na Emmanuel Twimanye

Wananchi waliodaiwa kuvamia  eneo la shule ya Msingi Kilabela Wilayani Sengerema  Mkoani  Mwanza  na kuendesha   shughuli za kilimo toka mwaka 2000  wameondolewa na ardhi hiyo kurejeshwa mikononi mwa shule hiyo.

Mgogoro huo umetatuliwa na katibu wa  Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema  Jamal  Athumani baada ya kufika katika eneo hilo na kusikiliza pande zote mbili kati ya wananchi waliodaiwa kuvamia eneo hilo na uongozi wa shule hiyo .

Sauti ya katibu wa  Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema  Jamal  Athumani

Mwalimu mkuu aliyewahi kuhudumu katika shule ya msingi kilabela  Deusdedith  Magafu Majula  amesema kuwa eneo la shule hiyo limetengwa toka mwaka 1993 na  kuvamiwa na wananchi hao mwaka  2000 .

Sauti ya Mwalimu mkuu mstaafu katika shule ya msingi kilabela  Mwl. Deusdedith  Magafu Majula

Diwani mstafu wa kata ya Sengerema ambaye kwa sasa ni katibu wa Mbunge wa Jimbo la Sengerema Levy Nghweli amesema kuwa eneo hilo ni mali halali ya shule .

Sauti ya katibu wa Mbunge wa Jimbo la Sengerema Levy Nghweli

Viongozi wa shule hiyo wamesema kuwa licha ya kulifikisha sakata hilo katika idara ya ardhi na vyombo vya dola  lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa .

Sauti ya Viongozi wa shule ya msingi kilabela wa sasa

Diwani wa kata ya Nyatukala  Mh,Michael Mchele na afisa mtendaji wa kata hiyo Hobokela  Masukila   wamewaomba wananachi kuacha tabia ya kuvamia maeneo ya shule .

Sauti ya Diwani wa kata ya Nyatukala  Mh,Michael Mchele na afisa mtendaji wa kata hiyo Hobokela  Masukila 

Mmoja wa wananchi wanaodaiwa kuvamia eneo hilo aliyefahamika kwa jina moja la Mzee Masatu alipotafutwa kwa njia ya simu   ili kuzungumzia suala hilo hakuwa  na sababu za msingi za kujieleza.

Sauti ya mzee Masatu mmoja ya wanaolalamikiwa kuvamia eneo la shule

Baadhi ya wananachi  wameitaja idara ya ardhi kuwa ni  chanzo cha kusababisha  migogoro ya ardhi katika jamii  kwa madai ya kupewa chochote  na  kuwatetea watu waliovamia maeneo    huku wakimshukuru katibu wa jumuiya ya wazazi kwa kutatua mgogoro huo.

Sauti za wananchi wanao ishi eneo jirani na shule ya Msingi Kilabela Sengerema

Naye  Afisa  ardhi wa Halmshauri ya wilaya ya Sengerema Saimon Mkalipa  amekiri mgogoro huo kufikishwa katika idara hiyo na kwamba  walikuwa wanaendelea kulishughulikia suala hilo.

Sauti ya Afisa  ardhi wa Halmshauri ya wilaya ya Sengerema Saimon Mkalipa