Sengerema FM

Wazazi washauriwa kuanzisha ujenzi wa hosteli

17 October 2023, 2:26 pm

Diwani wa kata ya Tabaruka Mh. Sospiter Busumabhu akizungumza kwenye mahafali shule ya sekondari Kijuka iliyopo kata ya Nyamazugo. Picha Elisha Magege

Shule ya sekondari Kijuka imeanzishwa mwaka 2012 kwa nguvu ya wananchi na serikali ambapo tangu kuanzishwa imekuwa ikifanya vibaya kitaaluma kutokana na wanafunzi kutembea umbali mrefu na kwa mwaka huu 2023 wamehitimu wanafunzi 42 kati ya wanafunzi 88 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2020.

Na. Elisha Magege.

Wazazi na walezi katika kijiji cha Kijuka kata ya Nyamazugo wameshauriwa kuanzisha ujenzi wa hosteli kwa nguvu zao ili kuwanusuru wanafunzi kumaliza masomo ya sekondari.

Ushauri huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Tabaruka Mh. Sospiter Busumabhu katika mahafali ya 9 ya kidato cha nne shule ya sekondari kijuka ambapo amesema ni aibu watoto kukatisha ndoto zao za kielimu kwa kupata ujauzito na kutembea umbali mrefu kulingana na mazingira ya vijijini.

Sauti ya diwani wa kata ya Tabaruka Sospiter Busumabhu akizungungumza kwenye mahafari ya 9 shule ya Sekondari Kijuka.

Kwa upande wao viongozi wa kijiji hicho wamesema wameupokea ushauri huo na kuahidi kuitisha kikao cha kujadili namna ya kuwanusuru watoto wao na adui Ujinga.

Sauti ya viongozi wa kijiji cha Kijuka Mwkt. ccm Thobias Watungala na mwenyekiti kijiji Thobias Mpiguji

Awali ikisomwa lisala kwa mgeni Rasimi mkuu wa shule Mwl. Patrick Buzinza Juvenary na Kisumo Lusobhangija Mwanafunzi mhitimu wamesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya utoro kwa wanafunzi jambo linalopelekea baadhi kushindwa kumaliza masomo yao.

Uongozi wa shule ukisoma risara kwa mgeni rasmi

Hata hivyo wazazi na walezi wmesema wapo tayali kujitolea kwa hali na mali ili kuwasaidia watoto kupata elimu kama ulithi wao wa hapo baadaye.

Sauti za wazazi na walezi wa wanafunzi shule ya Sekondari Kujuka

Zaidi ya wanafunzi 40 wameshindwa kumaliza masomo yao ya sekondari katika shule ya sekondari Kijuka kutokana na kutembea umbari mrefu na mimba za utotoni..