Sengerema FM

CCM Sengerema yaagiza kukamatwa fundi wa nyumba za walimu

13 February 2024, 5:09 pm

Wajumbe wa Kamati ya Sekretarieti ya chama cha mapinduzi ccm Wilaya ya Sengerema ikiwa kwenye moja ya majengo yaliyotelekezwa katika kata ya Nyamazugo. Picha na Emmanuel Twimanye

Kamati ya Sekretarieti ya ccm Wilaya ya Sengerema inafanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serkali ya awamu ya Sita, ambapo imekutana na changamoto ya Fundi aliyelipwa fedha na kushindwa kukamilisha majengo ya watumishi kisha kutokomea kusiko julikana.

Na:Emmanuel Twimanye

Wajumbe wa kamati ya Sekretarieti  ya  Chama cha Mapinduzi Wilayani Sengerema   Mkoani  Mwanza imeagiza kukamatwa fundi anayejenga nyumba za watumishi katika kata ya Nyamazugo Wilayani Sengerema  Mussa  Ntobi  kwa madai ya kutelekeza ujenzi huo na kutokomea kusikujulikana.

Wajumbe wa Kamati ya Sekretarieti ya chama cha mapinduzi ccm Wilaya ya Sengerema ikiwa kwenye moja ya majengo yaliyotelekezwa katika kata ya Nyamazugo. Picha na Emmanuel Twimanye

Kamati  hiyo imetoa agizo hilo baada ya kutembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi  katika kata hiyo unaojengwa kwa fedha za mfuko wa maendeleo ya jamii  (TASAF) na  kukuta ujenzi  umesimama   , huku fundi  akidaiwa kutokomea kusikojulikana   na kupelekea kukwamisha ujenzi huo.

Kufuatia  hali hiyo kamati hiyo imelazimika  kumpigia simu Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema  anayesimamia  mradi huo   Elias  Mwita  ili kujua nini kimekwamisha ujenzi huo .

Diwani wa kata ya Nyamazugo   Mh,Enock Sengerema na afisa mtendaji wa kata hiyo Elikana Ndiganya wameahidi kutekeleza maagizo ya kamati ya sekretarieti.

Katika hatua  nyingine   kamati hiyo  imeshauri  mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele kumwondoa afisa mtendaji  wa kata ya Nyamazugo katika katya hiyo Elikana Ndiganya kwa madai ya kushindwa kutimiza majukumu yake .

Aidha  kamati ya Sekretarieti  ya  Chama cha Mapinduzi Wilayani Sengerema imetembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika kata ya Nyamazugo ,Kasungamile pamoja na mradi wa ujenzi wa Bweni la wasichana katika kata ya Nyamatongo.